Mawasiliano na Usafirishaji
Halmashauri ya mji wa Mbinga inayo fursa ya uwekezaji katika eneo la usafirishaji kutokana na uwepo wa idadi kubwa ya watu wanao ingiza bidhaa za kibiashara na chakula. Hali ya barabara katika Mji wa Mbinga ni Nzuri tunayo barabara ya Lami inayo tokea Dar es salaam mpaka Mbinga. Pia eneo lote la Mji wa Mbinga lina Mtandao wa barabara ulio katika hali nzuri zinazopitika kwa vyombo mbalimbali vya usafiri katika majira yote ya Mwaka. Vile vile Halmashauri imetenga eneo la Kiwanja cha ndege lililopo eneo la Utiri kwa ajili ya usafiri wa anga. Katika upande wa Mawasiliano bado yapo maeneo mengi ambayo yanahitaji uwekezaji wa mawasiliano ya simu mfano maeneo ya Kihungu, Mpepai, Kagugu na Kitanda.
MBINGA
Sanduku la Barua: P.O.BOX 135
Simu ya Mezani: +225 - 2640664
Mobile: +225 – 2640664
Barua pepe: td@mbingatc.go.tz
Copyright ©2018 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.