Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe. Seleman Said Jaffo (Mb) baada ya kukagua na kuridhishwa na ujenzi wa jengo la Utawala la Halmashauri ya Mji wa Mbinga. Katika ziara yake ya siku moja Mjini hapa ,Mhe. Jaffo amesema kuwa Jengo hilo ni nzuri na ni mfano wa kuigwa kwani fedha zilitolewa na Serikali zimetumika Vizuri. Aidha Mhe. Jafo ametoa agizo kwa Wafanyakazi wa Halmashauri ya Mji kuhakikisha kuwa Ifikapo tarehe 30/01/2020 wote wawe wameingia katika jengo hilo kwani anaamini kuwa kazi za ukamilishaji wa jengo hilo zitaisha kwa wakati ikiwa mkataba unaonyesha mwisho ni tarehe 30/12/2019.
“…lakini hapa naomba niseme kazi hapa ni nzuri na mmepata Jengo nzuri sana na Halmashauri yenu itakuwa safi…na wengine waige mfano huu mnzuri, kwamba mnakuwa mnapewa fedha lakini mnazitumia vizuri, sio mnapewa fedha mnaleta ubabaishaji…” Alisema Mhe. Jaffo
MBINGA
Sanduku la Barua: P.O.BOX 135
Simu ya Mezani: +225 - 2640664
Mobile: +225 – 2640664
Barua pepe: td@mbingatc.go.tz
Copyright ©2018 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.